Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 40

Al-Israa 17:40

الإسراء

أَفَأَصْفَىٰكُمْ رَبُّكُم بِٱلْبَنِينَ وَٱتَّخَذَ مِنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنَـٰثًا ۚ إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا

Maana

Je, Mola wenu Mlezi amewateulia nyinyi wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakika nyinyi mnasema kauli kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Mola wenu Mlezi amekuteulieni wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakika nyinyi mnasema usemi mkubwa. [40]

[40] Subhanahu anayachukia wayasemayo makafiri kwamba Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Anasema: Mola wenu Mlezi amekufadhilisheni kuliko Mwenyewe kwa kukupeni nyinyi watoto wanaume wenye nguvu, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake kwa mnavyo dai? Kwa maneno yenu haya mnazua matusi makubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kwani Amewahusu nyinyi Mola wenu, enyi washirikina, kwa kuwapa watoto wa kiume na Yeye Akajichukulia kutokana na Malaika watoto wa kike? Neno lenu hili ni upeo wa ubaya na linachukiza sana, halinasibiani na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net