Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 41

Al-Israa 17:41

الإسراء

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِى هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ لِيَذَّكَّرُوا۟ وَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا نُفُورًا

Maana

Na tumekwishabainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tumekwisha bainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo. [41]

[41] Sisi tumebainisha katika Qur'ani hii kwa uwazi mzuri, tukipiga mifano na kutoa mawaidha na hukumu, ili wapate kwaidhika hawa washirikina. Lakini nyoyo zao zimekuwa kama mawe. Kubainisha huku hakukuwazidishia ila kuzidi kuwakimbiza na Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tumeeleza katika hii Qur’ani aina mbalimbali za hukumu, mifano na mawaidha, ili watu wapate kuwaidhika na kuzingatia yanayowafaa wayachukue na yenye kuwadhuru wayaache. Na haya maelezo na ufafanuzi hayawaongezei madhalimu isipokuwa kuwa mbali na haki na kughafilika kutia mambo akilini na kuzingatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net