Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 39

Al-Israa 17:39

الإسراء

ذَٰلِكَ مِمَّآ أَوْحَىٰٓ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ ٱلْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتُلْقَىٰ فِى جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا

Maana

Hayo ni katika hekima alizokufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, ukaja ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa. [39]

[39] Na hayo ni katika aliyo kufunulia Mola wako Mlezi, katika kuijua haki kwa dhati yake, na kheri ipate kutendwa. Wala usimfanyie Mwenyezi Mungu kuwa na mungu mwengine, usije kutupwa katika Jahannamu ukijilaumu na ukilaumiwa, umeangamia na umefurushwa mbali na rehema za Mola wako Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo tuliyoyaeleza na kuyafafanua kati ya hizi hukumu tukufu za kuamrisha matendo mema na kukataza tabia duni, ni miongoni mwa yale tuliyokutumia wahyi nayo. Na usimfanye, ewe binadamu, pamoja na Allah Mtukufu yoyote kuwa ni mshirika Wake katika kumuabudu, ukaja kutiwa ndani ya moto wa Jahanamu, hali ukilaumiwa na nafsi yako na watu, na ukawa ni mwenye kufukuzwa na kuepushwa na kila kheri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net