Al-Israa 17:30
الإسراءإِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرًۢا بَصِيرًا
Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona vyema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona. [30]
[30] Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha katika wao amtakaye. Kwani Yeye anawajua vyema tabia zao, na anaziona hali zao. Basi Yeye humpa kila mmoja wao, pindi akishika njia zake, kwa inavyo wafikiana na hikima yake Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Mola wako Anawakunjulia riziki baadhi ya watu na Anawapunguzia wengine kulingana na ujuzi Wake na hekima Yake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Yeye Ndiye Mwenye kuyaona mambo ya ndani ya waja Wake, hakuna chochote katika hali zao kilicho nje ya ujuzi Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net