Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 29

Al-Israa 17:29

الإسراء

وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ ٱلْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَّحْسُورًا

Maana

Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, ukabaki ukilaumiwa uliyefilisika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi. [29]

[29] Wala usiuzuilie mkono wako kutoa katika mambo ya kheri, ukaufanya kama ulio fungwa pingu za chuma shingoni mwako ukawa huwezi kuukunjua. Wala usiukunjue wote kabisa kwa kutumia ovyo. Utakuja tukanika kwa ubakhili na majuto, au utabaki huna kitu umefilisika kwa sababu ya ubadhirifu na israfu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala usiuzuie mkono wako kutumia katika njia njema, ukaidhiki nafsi yako na watu wako na wahitaji, na wala usipite kiasi katika matumizi ukatoa zaidi ya uwezo wako, kwani ukifanya hivyo utakua katika hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa, kwani watu watakulaumu na watakutukana, na ni mwenye kujuta juu ya ufujaji wako na mali yako kupotea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net