Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 28

Al-Israa 17:28

الإسراء

وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ٱبْتِغَآءَ رَحْمَةٍ مِّن رَّبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُل لَّهُمْ قَوْلًا مَّيْسُورًا

Maana

Na ikiwa utawapa mgongo sawasawa, nawe unatafuta rehema kutoka kwa Mola wako Mlezi unayoitaraji, basi sema nao maneno laini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao maneno laini. [28]

[28] Ukilazimika kujikurupusha na hao walio tajwa wenye haja, kwa sababu ya shida uliyo nayo, na ukawa hukuwapa kwa kuto kuwa nacho cha kuwapa sasa, na ilhali unataraji Mwenyezi Mungu atakufungulia baadae, basi nena nao kwa maneno mema ya kuwapa imani nawe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usipowapa hawa ambao uliamrishwa uwape, kwa kuwa hakuna kitu cha kuwapa, kwa kungojea riziki kutoka kwa Mola wako, basi waambie maneno laini ya upole kama vile kuwaombea dua awatajirishe na awape riziki kunjufu, na uwaahidi kwamba Allah Mtukufu Akiyafanya mambo ya riziki kuwa mepesi kwa wema Wake basi wewe utawapatia nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net