Al-Israa 17:27
الإسراءإِنَّ ٱلْمُبَذِّرِينَ كَانُوٓا۟ إِخْوَٰنَ ٱلشَّيَـٰطِينِ ۖ وَكَانَ ٱلشَّيْطَـٰنُ لِرَبِّهِۦ كَفُورًا
Hakika watumiao ovyo kwa fujo ni ndugu wa Mashetani. Na Shetani ni mwenye kumkufuru mno Mola wake Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi. [27]
[27] Kwani wabadhirifu (watumiaji ovyo) wenzao ni Mashetani, wanapokea minong'ono yao wanapo wachochea wafanye ufisadi na watumie kwa uharibifu. Na ni mtindo wa Shetani daima kukufuru neema ya Mola wake Mlezi. Na sahibu yake ni hali kadhaalika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale wenye kupita kiasi katika matumizi na wenye kutoa mali yao katika kumuasi Allah Mtukufu wanafanana na Mashetani kwenye uovu, uharibifu na maasia, na Shetani ni mwingi wa kukufuru, ni mkanushaji sana neema za Mola wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net