Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 26

Al-Israa 17:26

الإسراء

وَءَاتِ ذَا ٱلْقُرْبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلْمِسْكِينَ وَٱبْنَ ٱلسَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا

Maana

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. [26]

[26] Na wape jamaa zako haki yao kwa kuwafanyia wema na kuwaunga; na kadhaalika masikini mwenye haja, na msafiri aliye katikana na mali yake. Wape hao haki yao katika Zaka na sadaka, wala usiyavuruge mali yako kwa utumiaji ovyo usio na maslaha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na umfanyie wema kila mwenye ukaribu wa ujamaa na wewe, na umpe haki yake ya wema na hisani, na umpe masikini mwenye uhitaji na msafiri aliyekuwa mbali na watu wake na mali yake, na usitumie mali yako katika njia isiyokuwa ya kumtii Allah Mtukufu au kwa njia ya kupita kiasi na ufujaji.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net