Al-Israa 17:25
الإسراءرَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِى نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا۟ صَـٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلْأَوَّٰبِينَ غَفُورًا
Mola wenu Mlezi anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanaorudi sana kwake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake. [25]
[25] Enyi watu! Mola wenu Mlezi anajua kuliko nyinyi yaliyomo katika dhamiri zenu, na atakuhasibuni kwayo kwa thawabu na i'kabu. Na mkiwa mnakusudia wema na mkautenda, tena mkatokea baadhi yenu mkateleza, na kisha mkarejea kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Subhanahu atakusameheni. Kwani Yeye ni Mwenye kusamehe daima kwa wale wanao rejea kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mola wenu, enyi watu, ni Mjuzi zaidi wa mazuri na mabaya yaliyomo ndani ya nyoyo zenu. Iwapo matakwa yenu na makusudio yenu ni kumridhisha Allah Mtukufu na kujikaribisha Kwake, basi Yeye, kutakasika na sifa mbaya ni Kwake, kwa wenye kurejea Kwake katika nyakati zote ni Mwingi wa kusamehe. Basi yoyote yule ambaye Allah Mtukufu Amejua kwamba hakuna katika moyo wake isipokuwa ni kurejea Kwake na kumpenda, Yeye Atamsamehe yatakayotukia miongoni mwa madhambi madogo yanayolingana na tabia za kibinadamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net