Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 31

Al-Israa 17:31

الإسراء

وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَوْلَـٰدَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَـٰقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْـًٔا كَبِيرًا

Maana

Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao kulikuwa ni kosa kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa. [31]

[31] Ikiwa yaliyo khusiana na riziki yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, basi haikufaliini kuwauwa watoto wenu kwa kukhofu ufakiri utao weza kutokea. Kwani Sisi ni Wenye kudhamini riziki zao na riziki zenu. Hakika kuwauwa hao ni dhambi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkijua kwamba riziki iko kwenye mkono wa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, basi msiwaue watoto wenu kwa kuchelea umasikini, kwani Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Mwenye kuwaruzuku waja Wake, Anawaruzuku watoto kama Anavyowaruzuku wazazi. Hakika kuua watoto ni dhambi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net