Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 22

Al-Israa 17:22

الإسراء

لَّا تَجْعَلْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا

Maana

Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, ukaja ukawa wa kulaumiwa uliyetupika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika. [22]

[22] Ewe mwenye jukumu! Usimfanyie Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika, utakuja fedheheka kwa kudharauliwa, na utajaaliwa uwe mwenye kutupika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Usimfanye, ewe mwanadamu, pamoja na Allah Mtukufu mshirika yoyote katika ibada Yake, kwani ukifanya hivyo utarudi uwe ni mwenye kutukanika na kudhalilika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net