Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 21

Al-Israa 17:21

الإسراء

ٱنظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْـَٔاخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَـٰتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا

Maana

Angalia vipi tulivyowafadhilisha baadhi yao kuliko wengine wao. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi. [21]

[21] Hebu angalia kwa kuzingatia vipi tulivyo wafadhilisha baadhi ya waja wetu kuliko wengine, kwa kuwapa mali na vyeo na nafasi, pindi wakishika njia za kuyapata hayo katika dunia. Na hayo ni kwa hikima tunayo ijua Sisi. Na tafauti zao katika Akhera ni kubwa zaidi kuliko tafauti zao za duniani. Kwa hivyo yatakikana waishughulikie Akhera, kwani huko ndiko kwenye kutukuka kwa kweli na kuzidiana kwa hakika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Zingatia ewe Mtume, vile Allah Mtukufu Alivyowatukuza baadhi ya watu juu ya wengine ulimwenguni kiutajiri na kimatendo. Na Akhera ina daraja kubwa zaidi kwa Waumini na ina matukuzo makubwa zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net