Al-Israa 17:20
الإسراءكُلًّا نُّمِدُّ هَـٰٓؤُلَآءِ وَهَـٰٓؤُلَآءِ مِنْ عَطَآءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَآءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا
Wote hao tunawakunjulia, hawa na hao, katika vipawa vya Mola wako Mlezi. Wala vipawa vya Mola wako Mlezi havizuiliki.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wote hao tunawakunjulia - hawa na hao - katika neema za Mola wako Mlezi. Wala neema za Mola wako Mlezi hazizuiliki. [20]
[20] Na Sisi tutawakunjulia neema za Mola wako Mlezi hapa duniani makundi yote mawili, pindi wakichukua khatua ya kufikia hayo. Wala neema za Mola wako Mlezi hatonyimwa yeyote, akiwa Muumini au akiwa kafiri, maadamu wakishika njia za kuzitafuta.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kila kundi, miongoni mwa wenye kuufanyia kazi ulimwengu wenye kumalizika na wenye kuifanyia kazi Akhera yenye kusalia, tunalipatia riziki yetu: tunawaruzuku waumini na makafiri ulimwenguni. Kwani riziki inatokana na vipawa vya Mola wako kwa wema Wake; na vipawa vya Mola wako hanyimwi mtu yoyote, awe ni Muumini au ni kafiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net