Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 19

Al-Israa 17:19

الإسراء

وَمَنْ أَرَادَ ٱلْـَٔاخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا

Maana

Na anayeitaka Akhera, na akaifanyia juhudi ipasavyo ilhali ni Muumini, basi hao juhudi zao zitakuwa ni za kushukuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a'mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa. [19]

[19] Na mwenye kuitaka Akhera kwa vitendo vyake, naye akawa navyo hivyo vitendo, na akawa anamuamini Mwenyezi Mungu na malipo yake, basi watu kama hao vitendo vyao vitakubaliwa na Mwenyezi Mungu na watapata malipo kwa ajili yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yoyote aliyekusudia kwa matendo yake mema kupata malipo ya Nyumba ya Akhera yenye kusalia na akajishughulisha nayo kwa kumtii Allah Mtukufu Aliyetukuka, na hali yeye ni mwenye kumuamini Allah Mtukufu na kuamini thawabu Zake na malipo Yake makubwa, basi hao matendo yao ni yenye kukubaliwa ni yenye kuhifadhiwa kwa ajili yao mbele ya Mola wao na watapata malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net