Al-Israa 17:18
الإسراءمَّن كَانَ يُرِيدُ ٱلْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُۥ فِيهَا مَا نَشَآءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُۥ جَهَنَّمَ يَصْلَىٰهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا
Anayetaka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea humo (duniani) tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu, ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa. [18]
[18] Mwenye kutaka starehe za dunia hii ipitayo na akazitumikia kwa kutafutia kisingizio, wala asiwe na yakini na miadi, na wala asingojee malipo ya Akhera, tutamletea haraka haraka tuyatakayo ya duniani kwa ukunjufu na wasaa. Haya ni kwa tumtakaye kumletea haraka. Kisha tutamuandalia kwa Akhera Jahannamu ahilikike kwa joto lake, naye hali awe ni mwenye kushutumiwa kwa aliyo yatenda, mwenye kutengwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yoyote ambaye matakwa yake ni ulimwengu huu wa sasa na akaushughulikia huo peke yake, asiiamini Akhera na asifanye matendo ya kumfaa huko, Allah Mtukufu Atamharakishia, hapa ulimwenguni, Anayoyataka Allah Mtukufu na kuyapendelea miongoni mwa yale aliyoyaandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Mahfûḍ) kisha Allah Mtukufu Atamjaalia huko Akhera moto wa Jahanamu, atauingia akiwa ni mwenye kulaumiwa, ni mwenye kufukuzwa kwenye rehema Yake Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka. Hiyo ni kwa sababu ya kutaka kwake ulimwengu na kujishughulisha nao bila ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net