Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 23

Al-Israa 17:23

الإسراء

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ ٱلْكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

Maana

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata, "Ah!" Wala usiwakemee. Na uwaambie maneno ya heshima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. [23]

[23] Na Mola wako Mlezi amehukumu kuwa msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye. Na pia muwafanyie wema kwa ukamilifu wazazi wenu wawili. Na hao, au mmoja wao, wakifikilia kwako hali ya unyonge na mwisho wa umri wao, basi lisikutoke tamko la kuchoka nao au kuudhika kwa yanayo kupata kutokana nao. Wala usiwahamakie. Na nena nao maneno mazuri, laini, yenye kuwaonyesha ihsani na kuwahishimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako, ewe mwanadamu, Ameamrisha na kupasisha Apwekeshwe, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwa kuabudiwa Peke Yake, na Ameamrisha kuwafanyia wema baba na mama, hasa wakiwa katika hali ya ukongwe: usione dhiki wala uzito kwa jambo lolote ulionalo kwa mmoja wao au kwa wao wawili, wala usiwasikilizishe neno baya, hata kama ni sauti ya kuonesha kutoridhika ambayo ni neno baya la daraja ya chini kabisa, wala usiwafanyie tendo baya, lakini kuwa mpole kwao na uwaambie wao daima maneno mepesi yenye ulaini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net