Al-Israa 17:15
الإسراءمَّنِ ٱهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِى لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا
Anayeongoka, basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anayepotea, basi anapotea kwa hasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumtume mtume.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. [15]
[15] Mwenye kufuata njia ya Haki basi anajifaa mwenyewe, na mwenye kuiacha basi anajipoteza mwenyewe. Wala hapana mwenye kubeba dhambi zake akambebea dhambi za mwenginewe. Wala haitufalii kumuadhibu yeyote kwa kutenda kitu kabla hatujampelekea Mtume kutoka kwetu amwonyeshe njia ya Haki na kumkataza maovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kuongoka akafuata njia ya haki, basi malipo mema yake yatamrudia yeye peke yake; na mwenye kupotoka akafuata njia ya ubatilifu, basi mateso ya kufanya hivyo yatamrudia yeye peke yake; na hakuna nafsi yoyote iliyofanya dhambi itabeba makosa ya nafsi nyingine iliyofanya dhambi. Na Allah Mtukufu Hatamuadhibu yoyote isipokuwa baada ya kumsimamishia hoja kwa kutuma Mitume na kuteremsha Vitabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net