Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 14

Al-Israa 17:14

الإسراء

ٱقْرَأْ كِتَـٰبَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ ٱلْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا

Maana

Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu. [14]

[14] Ataambiwa: Soma kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa duniani alikuwa hajui kusoma. Soma kitabu cha a'mali zako. Hicho leo kinatosha kukuhisabia na kukudhibitia vitendo vyako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ataambiwa, «Soma kitabu cha matendo yako.» Hapo atasoma, hata kama hakuwa akijua kusoma ulimwenguni, «Leo nafsi yako itakutosheleza kuwa ni yenye kukuhesabia matendo yako, upate kujua malipo yake.» Huu ni miongoni mwa uadilifu na uchungaji haki mkubwa kabisa kwamba mja aambiwe, ‘jihesabu nafsi yako, kwani inatosha kuwa ni yenye kukuhesabu.’

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net