Al-Israa 17:13
الإسراءوَكُلَّ إِنسَـٰنٍ أَلْزَمْنَـٰهُ طَـٰٓئِرَهُۥ فِى عُنُقِهِۦ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُۥ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ كِتَـٰبًا يَلْقَىٰهُ مَنشُورًا
Na kila mtu tumemfungia matendo yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta ki wazi kimekunjuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa. [13]
[13] Na kila mtu tumemfungamanisha na a'mali yake, vitendo vyake, kama koja lilioko shingoni. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu kilicho andikwa vitendo vyake vyote. Atakiona kitabu hicho kiwazi iwe wepesi kwake kukisoma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kila binadamu Allah Mtukufu Anayajaalia yale anayoyatenda, yawe mema au maovu, ni yenye kuwa na yeye wakati wote, hatahesabiwa kwa matendo ya mtu mwingine, wala mwingine hatahesabiwa kwa matendo yake yeye. Na Allah Mtukufu Atamtolea, Siku ya Kiyama, kitabu kilichoandikwa ndani yake yale aliyoyatenda; atakiona kimefunguliwa mbele yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net