Al-Israa 17:12
الإسراءوَجَعَلْنَا ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ ءَايَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَآ ءَايَةَ ٱلَّيْلِ وَجَعَلْنَآ ءَايَةَ ٱلنَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا۟ فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ وَلِتَعْلَمُوا۟ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلْحِسَابَ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ فَصَّلْنَـٰهُ تَفْصِيلًا
Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na ili mpate kujua idadi ya miaka na hesabu. Na kila kitu tumekifafanua kwa kina waziwazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi. [12]
[12] Na Sisi tumejaalia usiku na mchana, kwa namna yao na kupishana kwao, kuwa ni alama zenye kuonyesha Upweke wetu na Uwezo wetu. Tukauondoa mwangaza kwenye usiku, na kisionekane kitu. Na alama yake ni giza liso kuwa na jua. Hiyo ni ishara kubwa. Na mchana tukaufanya wa kuangaza. Hapo laonekana jua, ile ishara kuu, ili mpate kwenda mtakako wakati huo katika kutafuta maisha yenu. Na katika kuja usiku na mchana mpate kujua idadi ya miaka na hisabu za miezi na siku. Na Sisi tumekubainishieni kila kitu kwa uwazi kwa sababu ya maslaha yenu, ili isimame hoja juu yenu baada kutimia neema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumefanya usiku na mchana kuwa ni alama mbili zenye kuonyesha upweke wetu na uwezo wetu, tukaifuta alama ya usiku, nayo ni mwezi, na tukaifanya alama ya mchana, nayo ni jua, ni yenye mwangaza, ili binadamu apate kuona kwenye mwangaza wa mchana namna ya kuendesha mambo ya maisha yake na ili aingie kwenye utulivu na mapumziko wakati wa usiku, na ili watu wajue, kwa kupishana mchana na usiku, idadi ya miaka na hesabu ya miezi na siku, wakaweka juu ya hiyo mipango wanayoitaka ya maslahi yao. Na kila kitu tumekifafanua ufafanuzi wa kutosha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net