Al-Israa 17:11
الإسراءوَيَدْعُ ٱلْإِنسَـٰنُ بِٱلشَّرِّ دُعَآءَهُۥ بِٱلْخَيْرِ ۖ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ عَجُولًا
Na mtu huomba maovu kama vile aombavyo heri, kwani mtu ni mwenye pupa mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa. [11]
[11] Ni katika tabia ya mwanaadamu kufanya haraka katika kuwahukumia watu kwa yanayo wapata, na katika kauli zake na vitendo vyake. Naye hukimbilia kulingania shari kama anavyo lingania kheri. Naye hufanya haraka kumuapiza kwa Mwenyezi Mungu amteremshia shari yule aliye mkasirisha, kama anavyo fanya haraka kuomba kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na binadamu wakati mwingine hujiapiza mabaya nafsi yake au mtoto wake au mali yake awapo na hasira kama vile anavyoomba mema. Hii ni kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu na pupa lake. Na miongoni mwa rehema za Allah Mtukufu kwake ni kwamba Yeye Anayakubali maombi yake mema na sio mabaya na kwamba Yeye anajua kuwa yeye hakukusudia kutaka hilo. Hakika binadamu ana tabia ya kuwa na pupa sana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net