Al-Israa 17:16
الإسراءوَإِذَآ أَرَدْنَآ أَن نُّهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا۟ فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا ٱلْقَوْلُ فَدَمَّرْنَـٰهَا تَدْمِيرًا
Na pindi tukitaka kuuteketeza mji, tunawaamrisha wale wana starehe na taanusi wake, lakini wao wakaendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli ikathibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa. [16]
[16] Na pindi tukikadiria tangu azali katika Lauhun-mahfuudh kuwateketeza watu wa mji fulani kwa mujibu wa hikima yetu, basi Sisi huwasalitisha wale walio jidekeza kwa taanusi katika huo mji, wakafanya fisadi zao, wakaacha njia ya Haki, na wakawafuata wenginewe bila ya kutambua, na kwa hivyo huo mji wote tena hapo hustahiki kuangamizwa. Nasi huuangamiza vikubwa mno!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulipo taka kuwaangamiza watu wa mji kwa udhalimu wao, tuliwaamrisha viongozi wake wamtii Alla na wampwekeshe na wawaamini Mitume Wake, na wasiokua wao wako nyuma yao kwa kuwafuata, wakaasi amri ya Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake, hapo likapasa juu yao neno la adhabu ambalo hakuna namna ya kurudishwa, na tukawamaliza kwa maangamivu yaliyotimia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net