Al-Israa 17:106
الإسراءوَقُرْءَانًا فَرَقْنَـٰهُ لِتَقْرَأَهُۥ عَلَى ٱلنَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَـٰهُ تَنزِيلًا
Na Qur-ani tumeigawanya sehemu mbalimbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Qur'ani tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo. [106]
[106] Na hii Qur'ani tumeigawa na tumeiteremsha kipande kipande kwa muda mrefu, ili uwasomee watu kwa taratibu wapate kuifahamu. Tumeiteremsha kidogo kidogo kwa utulivu bila ya matatanisho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumekuteremshia, ewe Mtume, Qur’ani tuliyoieleza, tukaipanga na kuifafanua ikawa ni yenye kutenganisha baina ya uongofu na upotevu na ukweli na ubatilifu, ili upate kuwasomea watu kwa umakinifu na upole; na tumeiteremsha mafungu mafungu kidogo kidogo kulingana na matukio ya wakati na mahitaji yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net