Al-Israa 17:105
الإسراءوَبِٱلْحَقِّ أَنزَلْنَـٰهُ وَبِٱلْحَقِّ نَزَلَ ۗ وَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا
Na kwa Haki tuliiteremsha, na kwa Haki iliteremka. Na hatukukutuma isipokuwa uwe mbashiri na mwonyaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na mwonyaji. [105]
[105] Na hatukuiteremsha Qur'ani ila kwa kuunga mkono hikima ya Mwenyezi Muungu, iliyo pelekea kuteremshwa kwake. Nayo hiyo Qur'ani kwa dhati yake haikuteremka ila kuwa imekusanya Ukweli wote. Kwani itikadi zake ndizo zilizo sawa, na hukumu zake ndizo zilizo nyooka. Na wewe, ewe Nabii, hatukukutuma ila uwe mbashiri wa kuwabashiria Pepo wenye kuamini, na mwonyaji kuwaonya wanao ukanya Moto. Basi wewe huna jukumu lolote ikiwa wao hawaamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumemteremshia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), hii Qur’ani ili kuwaamrisha waja, na kuwakataza maovu nakuwalipa mema na kuwaadhibu; na imeteremka kwa ukweli, uadilifu na utunzi isibadilishwe na isigeuzwe. Na hatukukutuma wewe, ewe Mtume, isipokuwa ni uwabashirie Pepo waliotii na uwaonye na Moto walioasi na kukanusha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net