Al-Israa 17:104
الإسراءوَقُلْنَا مِنۢ بَعْدِهِۦ لِبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱسْكُنُوا۟ ٱلْأَرْضَ فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ ٱلْـَٔاخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا
Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili, "Kaeni katika nchi. Na itakapokuja ahadi ya Akhera, tutawaleta nyote pamoja."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi. Itapo kuja ahadi ya Akhera tutakuleteni nyote pamoja. [104]
[104] Tukamvua Musa na kaumu yake, na baada ya kumzamisha Firauni tukasema kuwaambia Wana wa Israili: Kaeni katika nchi takatifu ilioko Sham. Ukija wakati wa uhai wa pili tutakutoeni makaburini kwenu kwa mchanganyiko. Kisha tutakuhukumuni kwa uadilifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukasema, baada ya kuangamia Fir’awn na askari wake, kuwaambia Wana wa Isrãîl, «Kaeni ardhi ya Shãm. Na itakapo kuja Siku ya Kiyama, tutawaleta nyote kutoka makaburini mwenu kufika kwenye kisimamo cha kuhesabiwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net