Al-Israa 17:103
الإسراءفَأَرَادَ أَن يَسْتَفِزَّهُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ جَمِيعًا
Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha majini yeye na wale waliokuwa pamoja naye wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na walio kuwa pamoja naye wote. [103]
[103] Firauni akashikilia uasi wake, akataka kumtoa Musa na Wana wa Israili katika nchi ya Misri. Tukamzamisha yeye na askari wake wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo Fir‛awn akataka kumbabaisha Mûsã na kumtoa pamoja na Wana wa Isrãîl kwenye ardhi ya Misri, tukamuangamiza baharini yeye na askari waliokuwa pamoja na yeye kwa kuwatesa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net