Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 107

Al-Israa 17:107

الإسراء

قُلْ ءَامِنُوا۟ بِهِۦٓ أَوْ لَا تُؤْمِنُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ مِن قَبْلِهِۦٓ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا

Maana

Sema, "Iaminini au msiiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika wale walio pewa ilimu kabla yake, wanapo somewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu. [107]

[107] Waambie makafiri wa Makka kwa kuwatisha: Jichagulieni nafsi zenu mlitakalo - kuiamini Qur'ani au la! Kwani hakika walio pewa ilimu sawa na fahamu baraabara kabla ya kuteremka kwake, wakisomewa Qur'ani huangukia kwenye nyuso zao kwa kusujudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa wakanushaji, Iaminini Qur’ani au msiiamini, kwani kuiamini kwenu hakuiongezei ukamilifu, na kuikanusha kwenu hakuifanyi iwe na upungufu, kwani wanavyuoni waliopewa Vitabu vilivyotangulia kabla ya Qur’ani na wakajua uhakika wa wahyi, wanaposomewa Qur’ani wananyenyekea na wanamsujudia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa nyuso zao kwa kumtukuza na kwa kumshukuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net