Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 66

An-Nahl 16:66

النحل

وَإِنَّ لَكُمْ فِى ٱلْأَنْعَـٰمِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِى بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَآئِغًا لِّلشَّـٰرِبِينَ

Maana

Na hakika katika wanyama wa kufugwa[1], mna mazingatio. Tunawanywesha katika vile vilivyomo matumboni mwao - baina ya mavi na damu - maziwa safi, mazuri kwa wanywao.

[1] Nao ni ngamia, ng'ombe, mbuzi na kondoo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi mazuri kwa wanywao. [66]

[66] Na enyi watu! Hakika katika nyama hoa, yaani mifugo, ngamia, ng'ombe, na kondoo na mbuzi, mna mawaidha yanayo faa kuzingatiwa na kufuatwa uwongofu wake wa kumtoa mtu ujingani akaingia kumjua Mwenye kuumba, Aliye anzisha kila kitu, Mwenye hikima. Na Sisi tunakunywesheni kutokana na baadhi ya viliomo matumboni mwa hao wanyama vilio zidi katika chakula na damu maziwa safi, matamu, mepesi kuyapata kwa wanao kunywa. Katika viwele vya wanyama wa mifugo imo namna ya mitoki (glands) ambayo inachuja maziwa. Mitoki hiyo inanyweshwa na mishipa inayo leta madda maalumu kutokana na damu, na (chyle); hicho ni chakula kilicho tayarishwa. Viwili hivyo huwa vimekwisha lainishwa kwa kumezwa kama ni chakula. Kisha hapo hizo glands za maziwa huteuwa sehemu yenye kuhitajiwa kwa kufanya maziwa kutokana na vitu viwili hivyo, damu na chyle, na humiminiwa maji maalumu kugeuza hivyo vikawa maziwa yenye kukhitalifiana na asili yake kwa rangi na utamu kabisa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa kweli muna nyinyi, enyi watu, mazingatio katika wanyama howa, nao ni ng’ombe, ngamia na mbuzi na kondoo. Kwani mumeshuhudia kwamba sisi tunawanywesha kutoka kwenye nyato zao maziwa yanayotoka kati ya choo, kilicho ndani ya tumbo, na damu yakiwa yamesafishika na kila uchafu, yenye ladha, hayamkeri mwenye kuyanywa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net