Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 67

An-Nahl 16:67

النحل

وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلْأَعْنَـٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Maana

Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza vileo na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili. [67]

[67] Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu tuliyo kuneemesheni kwayo na tukakuwezesheni kuitumia, mnakamua maji yake yakatoka ulevi usio kuwa mzuri, na chakula kilicho kuwa kizuri. Hakika katika haya pana alama yenye kuonyesha uwezo na rehema kwa watu wanao nafiika kwa akili zao. (Kitu kile kile kina faida kikitumiwa kwa sharia za Mwenyezi Mungu za maumbile, na kile kile kikawa na madhara kikitumiwa kinyume na hizo sharia.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa neema zetu kwenu ni yale matunda ya mitende na mizabibu mnayoyachukuwa mkayatengeneza pombe yenye kulewesha - na hii na kabla haijaharamishwa- na chakula kizuri. Hakika katika hayo yaliyotajwa pana ushahidi juu ya uwezo wa Allah Mtukufu kwa watu wenye kuzitia akilini hoja hizo wakazizingatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net