An-Nahl 16:65
النحلوَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَحْيَا بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَآ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ
Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika, katika hayo imo Ishara kwa kaumu wanaosikia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika katika hayo imo Ishara kwa watu wanao sikia. [65]
[65] Na Mwenyezi Mungu ameteremsha kutoka mbinguni maji yanayo bebwa na mawingu, akaifanya ardhi ikamea na ikawa na uhai, baada ya kuwa kabla yake kavu haina uhai. Hakika katika hayo pana dalili wazi ya kuwepo Mwenye kudabiri Mwenye hikima. Maji huteremka kutoka mbinguni kuangukia ardhini, na huko huyayusha chumvi chumvi zake za namna mbali mbali ambazo hunyonywa na mimea kugeuka kwenye uhai.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Ameteremsha mvua kutoka mawinguni, na Akatoa kwa mvua hiyo mimea kutoka ardhini baada ya kuwa kame na kavu. Hakika katika kuteremsha mvua na kuotesha mimea pana ushahidi juu ya uwezo wa Allah Mtukufu wa kufufua, na pia pana ushahidi juu ya upweke Wake kwa watu wanaosikia, wanaozingatia, wanaomtii Allah Mtukufu na wanaomuogopa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net