An-Nahl 16:63
النحلتَٱللَّهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَعْمَـٰلَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Tallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini Shetani akawapambia matendo yao. Kwa hivyo leo, yeye ndiye kipenzi chao msaidizi, nao wana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako,lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata adhabu chungu. [63]
[63] Ewe Nabii! Jua kwa yakini kwamba Sisi tuliwatuma Mitume kabla yako kwa kaumu nyingi kama tulivyo kutuma wewe kwa watu wote. Lakini Shetani aliwapambia ukafiri, na ushirikina, na maasi. Basi wakawakanya Mitume wao, na wakawaasi, na wakamsadiki Shetani na wakamt'ii yeye. Basi yeye amekuwa ndiye mwenye kuyatawala mambo yao katika dunia, akiwapambia mambo ya kuwadhuru. Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Naapa kwa Allah Mtukufu, hakika tumewapeleka Mitume kwa makundi ya watu kabla yako, ewe Mtume, Shetani akawapambia matendo waliyoyafanya ya ukafiri, ukanushaji na kuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu. Yeye anasimamia kazi ya kuwapoteza wao ulimwenguuni, na hao wenye kupotezwa, watakuwa na adhabu kali yenye kuumiza kesho akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net