Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 62

An-Nahl 16:62

النحل

وَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ ٱلْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ

Maana

Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyovichukia wao, na ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mazuri zaidi. Hakuna shaka kwamba hakika wana Moto, na kwamba kwa yakini wataachwa humo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyo vichukia wao, na ndimi zao zinasema uwongo kwamba wao watapata mema. Hapana shaka hakika wamewekewa Moto, nao wataachwa humo. [62]

[62] Na washirikina wanamnasibisha Mwenyezi Mungu mabinti na ushirika mambo ambayo wao wanayachukia. Na ndimi zao zinatamka uwongo wanapo dai ya kwamba, kama walivyo kuwa na utajiri na utawala duniani, basi kadhaalika Akhera nao watapata malipo mema kwa Mwenyezi Mungu watapo fufuliwa; nayo ni Pepo! Hapana shaka hao watatiwa Motoni, nao watasukumwa huko kabla ya wengineo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa maovu yao, ni kwamba wao wanawafanya ni wa Allah Mtukufu watoto wa kike ambao wao wenyewe wanawachukia. Na ndimi zao zinasema urongo kwamba wao watakuwa na mwisho mwema. Kwa kweli, wao watakuwa na Moto na wao ni wenye kuachwa humo na kusahauliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net