Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 61

An-Nahl 16:61

النحل

وَلَوْ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَآبَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَـْٔخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha juu yake hata mnyama mmoja. Lakini anawaahirisha mpaka muda uliowekwa. Na unapofika muda wao, hawatakawia hata saa moja wala hawatatangulia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa mujibu wa dhulma zao, basi asingeli mwacha hapa hata mnyama mmoja. Lakini anawaakhirisha mpaka muda ulio wekwa. Na unapo fika muda wao hawatakawilia hata saa moja wala hawatatangulia. [61]

[61] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli fanya haraka kuwaadhibu watu kwa dhulma zao wanazo zifanya, basi asingeli mwacha hata mnyama mmoja juu ya ardhi. Lakini Yeye kwa upole wake na hikima yake anawaakhirisha madhaalimu mpaka wakati aliyo uweka, nao ndio wakati utapo kwisha muda wao. Ukija wakati huo hawato taakhari hata kidogo, wala hawato tangulia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau kwamba Allah Mtukufu Anawapatiliza watu kwa ukafiri wao na uzushi wao, Asingemuacha juu ya ardhi mtu yoyote mwenye kutembea, lakini Anawabakisha mpaka wakati uliopangwa, nao ni mwisho wa muda wao wa kuishi, basi utakapofika wakati wao wa kuondoka duniani, hawatacheleweshwa nao hata muda mchache wala hawatautangulia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net