An-Nahl 16:60
النحللِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوْءِ ۖ وَلِلَّهِ ٱلْمَثَلُ ٱلْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Wale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [60]
[60] Ni hali mbaya ya wasio amini Akhera na yote yaliyoko huko ya thawabu na adhabu, nayo ni ile haja ya kutaka watoto wa kiume na kuchukia watoto wa kike. Na Mwenyezi Mungu ana sifa tukufu. Yeye ni Mkwasi, hahitajii kitu, wala hana haja ya mtoto. Naye ni Mwenye kushinda, Mwenye nguvu, wala hana haja ya msaidizi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wasioiamini Akhera na wasiofanya matendo ya kuwafaa huko wana sifa mbaya za ulemevu, uhitaji, ujinga na ukafiri, na Allah Mtukufu Ana sifa tukufu za ukamilifu, kujitosheleza na viumbe Vyake. Na Yeye Ndiye Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwenye hekima katika uendeshaji Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net