An-Nahl 16:59
النحليَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلْقَوْمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓ ۚ أَيُمْسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُۥ فِى ٱلتُّرَابِ ۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ
Anajificha asionekane na watu kwa sababu ya ubaya wa yule aliyebashiriwa! Je, akae naye pamoja na fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama, ni ubaya mno wanavyohukumu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je,akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyohukumu! [59]
[59] Anajaribu kujificha watu wasiione huzuni ya machungu yaliyo mpata kwa kupewa khabari ya binti aliye zaliwa. Anatapatapa: amwache hai juu ya fedheha anayo iona, kama anavyo jigamba? Au amzike katika udongo naye yuhai mpaka afe? Ewe msikilizaji! Zingatia uwovu wa vitendo vya watu hawa! Na uovu gani wa kumhukumia Mwenyezi Mungu mabinti ambao wao wanawachukia!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Anajificha kwa kuchukia asionekane na watu wake, akiona aibu na kuingiwa na huzuni kwa habari iliyomchukiza ya kuzaliwa mtoto wa kike, huku akiwa ameduwaa juu ya tukio la mtoto huyo aliyezaliwa: je, amuache kuishi kwenye hali ya unyonge na udhalili au amzike mchangani akiwa hai? Jueni mtanabahi kwamba ni uamuzi mbaya mno wanaouamua wa kuwafanya watoto wa kike ni wa Allah Mtukufu na watoto wakiume ni wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net