An-Nahl 16:54
النحلثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ
Na anapowaondoshea madhara hayo, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi, [54]
[54] Kisha akiitikia maombi yenu na akakuondoleeni madhara baadhi yenu huisahau Haki ya Mwenyezi Mungu ya Umoja wake na kumsafia ibada Yeye tu, wakamshirikisha Muumba wao na Mlezi wao, na wakawaabudu naye wenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha anapowaondolea matatizo na magonjwa, kutahamaki linatoka kundi la watu miongoni mwenu wakawa wanawafanya asiyekuwa Yeye kuwa ni washirika pamoja na Yeye na wategemewa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net