An-Nahl 16:53
النحلوَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ ٱللَّهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْـَٔرُونَ
Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakiwagusa madhara, mnamyayatikia Yeye.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye. [53]
[53] Na neema yoyote ikikujieni, basi inatoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kisha kikikupateni chochote cha kukudhuruni msiyayatike kwa ukomo wa kelele zenu kwa mwenginewe yeyote isipo kuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na neema yoyote mliyonayo ya uongofu au afya ya mwili, ukunjufu wa riziki na watoto na yasiyokuwa hayo, inatoka kwa Allah Mtukufu Peke Yake, Yeye Ndiye Mwenye kuwaneemesha nayo. Kisha yanapowapata magonjwa, matatizo na ukame, basi ni kwa Allah Mtukufu Peke Yake mnalia kwa maombi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net