Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 52

An-Nahl 16:52

النحل

وَلَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ

Maana

Na ni vyake Yeye vilivyo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je, mnamcha mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni vyake Yeye viliomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je! Mtamcha mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu? [52]

[52] Yeye pekee ndiye mwenye vyote viliomo mbinguni na katika ardhi, kwa kuviumba na kuvimiliki na kumuabudu. Basi ni haki yake Yeye tu pekee kuabudiwa na kuhimidiwa na kunyenyekewa, na kutarajiwa rehema yake, na kuogopwa adhabu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ni vya Allah Mtukufu, Peke Yake, vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuviendesha. Na ibada inaelekezwa Kwake PekeYake, na pia kutiiwa na kutakaswa daima. Basi je, inafaa kwenu nyinyi mumuogope asiyekuwa Yeye na mumuabudu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net