An-Nahl 16:51
النحلوَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ إِلَـٰهَيْنِ ٱثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ فَإِيَّـٰىَ فَٱرْهَبُونِ
Na Mwenyezi Mungu amesema: Msijifanyie miungu wawili! Hakika Yeye ndiye Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni sana Mimi tu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu amesema: Msiwe na miungu wawili! Hakika Yeye ni Mungu Mmoja. Basi niogopeni Mimi tu! [51]
[51] Mwenyezi Mungu amesema: Msiabudu wawili, wala msifanye miungu wawili. Kwani kushiriki katika ibada kunapingana na Umoja wa kuumba. Wa kuabudiwa kwa Haki ni Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni Mimi wala msimkhofu mwengine.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na alisema Allah Mtukufu kuwaambia waja Wake, «Msiabudu waungu wawili, kwani muabudiwa wenu ni Mola Mmoja. Basi niogopeni mimi na sio mwingine asiyekuwa mimi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net