An-Nahl 16:50
النحليَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩
Vinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Vinamkhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa. [50]
[50] Na hali yao ni kuwa daima wamo katika kumkhofu Mola wao Mlezi, Mwenye uwezo na nguvu, na wanafanya anayo waamrisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao Malaika wanamuogopa Mola wao Ambaye Yuko juu yao kwa dhati Yake, utendeshaji nguvu Wake na ukamilifu wa sifa Zake, na wanafanya wanayoamrishwa ya kumtii Allah Mtukufu. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya kuwa Allah Mtukufu Yuko juu ya viumbe vyake vyote, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net