An-Nahl 16:49
النحلوَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ مِن دَآبَّةٍ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ
Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama mpaka Malaika na wala havitakabari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi, tangu wanyama mpaka Malaika, vinamsujuidia Mwenyezi Mungu, na wala havitakabari. [49]
[49] Ni kwa Mwenyezi Mungu pekee - wala si kwa mwenginewe - hunyenyekea na kut'ii vyote alivyo viumba mbinguni na viumbe viliomo na vyendavyo katika ardhi. Na mbele yao ni Malaika wanao nyenyekea wala hawatakabari na kumt'ii. Aya hii imeitangulia sayansi kwa kusema kuwa katika baadhi ya sayari upo uhai katika mfumo huu wetu wa jua, au nje yake. Sayansi sasa inajaribu kutaka kuvumbua hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na vinamsujudia Allah Mtukufu Peke Yake vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini, miongoni mwa vinavyotambaa. Na Malaika wanamsujudia Allah Mtukufu, na wao hawafanyi ujeuri kwa kukataa kumuabudu Yeye. Na Amewahusu Malaika kwa kuwataja baada ya kuwakusanya pamoja na viumbe wengine, kutokana na utukufu wao, ubora wao na wingi wa kuabudu kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net