An-Nahl 16:48
النحلأَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَىْءٍ يَتَفَيَّؤُا۟ ظِلَـٰلُهُۥ عَنِ ٱلْيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدًا لِّلَّهِ وَهُمْ دَٰخِرُونَ
Je, hawavioni vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu, vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, vikimsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawavioni vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu - vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, kumsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea? [48]
[48] Hao makafiri wameghafilika na Ishara za Mwenyezi Mungu zilizo wazunguka. Wala hawatazami wakazingatia vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu vilivyo tulia, na hali vivuli vyake vinakwenda. Mara vinanyookea kulia na mara kushoto, vikifuata mwendo wa jua mchana, na mwendo wa mwezi usiku. Na vyote hivyo vinat'ii amri ya Mwenyezi Mungu, vinafuata hikima ya mipango yake. Na lau washirikina wangeli zingatia haya, wangeli jua kuwa Muumba wake, na Mwenye kuyapanga ni Yeye peke yake anaye stahiki kuabudiwa na kunyenyekewa, Muweza wa kuwahiliki akitaka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, kwani makafiri hawa wamekuwa vipofu wakawa hawaangalii vitu vyenye vivuli Alivyoviumba Allah Mtukufu, kama vile majabali na miti ambayo vivuli vyake vinapinduka, mara nyingine upande wa kulia na mara nyingine upande wa kushoto, kufuatia mwendo wa jua kipindi cha mchana na mwendo wa mwezi kipindi cha usiku.Vyote hivyo ni vyenye kuunyenyekea ukuu wa Allah Mtukufu na utukufu Wake. Navyo viko chini ya uendeshaji Wake, mipango Yake na utendeshaji nguvu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net