An-Nahl 16:47
النحلأَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Au hatawashika huku wana hofu? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au hatawashika kwa kitisho na kuwapunguza kidogo kidogo? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu. [47]
[47] Au akawateremshia adhabu katika nafsi zao na mali yao kidogo kidogo, na hali wao kila wakati wa hiyo adhabu wamo katika khofu na kuingoja iwateremkie. Basi, enyi washirikina! Msiendelee, mkajidanganya kwa kuchelewa adhabu yenu! Upole wake Mwenyezi Mungu ulio enea, na rehema yake iliyo kunjuka, ndio iliyo hukumu asikuleteeni kwa haraka adhabu ya hapa duniani, ili mpate kufikiri na kuzingatia. Kwani Yeye Subhanahu ni Mpole na Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au Allah Mtukufu Awapatilize kwa upungufu wa mali na watu na matunda au katika hali ya kuogopa kwao Asiwatie mkononi? Kwani Mola wenu ni Mpole kwa waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net