Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 55

An-Nahl 16:55

النحل

لِيَكْفُرُوا۟ بِمَآ ءَاتَيْنَـٰهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا۟ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ

Maana

Wakizikataa neema tulizowapa. Basi stareheni. Mtakujajua!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakizikataa neema tulizo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! [55]

[55] Hayo hutokea ili mwisho wao huwa kuikanya fadhila yetu kwa yale tuliyo wapa. Basi enyi makafiri! Stareheni na hayo msiyo yatolea Haki ya shukrani. Mtakuja kuujua mwisho wa ukafiri!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ili wapate kuzikanusha neema zetu kwao, na miongoni mwazo ni kuondolewa matatizo. Basi jistarehesheni na ulimwengu wenu, nao mwisho wake ni kutoweka, hapo mtajua mwisho wa ukanushaji wenu na uasi wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net