An-Nahl 16:33
النحلهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Wanangojea jingine hawa isipokuwa Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi? Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanangojea jengine hawa ila Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi? Kama hivyo walitenda walio kuwa kabla yao. Na MwenyeziMungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe. [33]
[33] Hao ndio wachamngu walio jitengenezea Akhera yao. Na hayo ndiyo malipo yao. Ama washirikina kwa sababu ya inadi yao na kubakia kwao kwenye ushirikina wao, hawataraji ila Malaika waje kunyakua roho zao nao wamezidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na vitendo vya shari. Na itawajia adhabu ya Mola wako Mlezi iwateketeze wote. Na kama walivyo fanya makafiri hawa, basi walikwisha wafanyia Manabii wao wale walio watangulia, na Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa vitendo vyao. Wala Yeye hakuwadhulumu pale alipo waadhibu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao walipo zitia katika adhabu kwa ukafiri wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Washirikina hawangojei isipokuwa wajiwe na Malaika wazichukue roho zao wakiwa katika hali ya ukafiri, au ije ya amri ya Allah Mtukufu na adhabu ya haraka ya kuwaangamiza. Na kama walivyokanusha hawa, walikanusha makafiri kabla yao, Allah Mtukufu Akawaangamiza. Wala Allah Mtukufu Hakuwadhulumu kwa kuwaangamiza na kuwaadhibu, lakini wao ndio waliokuwa wakizidhulumu nafsi zao kwa mambo yaliyowafanya wastahili kuadhibiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net