An-Nahl 16:32
النحلٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمُ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri, wanawaambia: Salama iwe juu yenu! Ingieni Bustanini kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda. [32]
[32] Na ndio hao Malaika huzichukua roho zao na hali wamesafika na uchafu wa ushirikina na maasi. Na Malaika watawaambia kwa kuwatuza: Amani kwenu itokayo kwa Mwenyezi Mungu! Baada ya hii leo hamtopata la karaha. Na ifurahieni Pepo mtakayo ingia kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo vitanguliza katika dunia yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ambao Malaika watazichukua roho zao, na hali nyoyo zimetakasika na ukafiri. Malaika watawaambia, «Amani iwe juu yenu, Maamkizi yenu peke yenu, na muokoke na kila ovu, ingieni Peponi kwa yale mliyokuwa mkiyafanya ya kumuamini Allah Mtukufu na kufuata amri Yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net