An-Nahl 16:31
النحلجَنَّـٰتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَآءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِى ٱللَّهُ ٱلْمُتَّقِينَ
Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kwa chini yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kati yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha. [31]
[31] Nazo ni Bustani madhubuti za kudumu, zenye kupitiwa na mito chini ya majumba na miti yake. Na hao watapata kila neema waipendayo. Na mfano kama huu ndio malipo ya mema anayo walipa Mwenyezi Mungu wachamngu wote wanao muamini, na wakajikinga na yanayo mkasirisha, na wakavifanya vyema vitendo vyao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makazi yao ni mabustani ya Pepo ya Milele, watatulia humo, hawatatoka humo kabisa, mito itakuwa ikipita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari. Watakuwa na kila kinachotamaniwa na nafsi zao. Kwa mfano wa malipo haya mazuri, Allah Mtukufu Atawalipa wachamungu wenye kumuogopa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net