An-Nahl 16:30
النحلوَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا۟ خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ ٱلْمُتَّقِينَ
Na wataambiwa wale waliomcha Mungu: Mola wenu Mlezi aliteremsha nini? Watasema: "Heri." Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na ni njema mno nyumba hiyo ya wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wataambiwa walio mcha Mungu: Mola wenu Mlezi kateremsha nini? Watasema: Kheri. Walio fanya wema katika dunia hii watapata wema. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na njema mno nyumba ya wachamngu. [30]
[30] Na walio muamini Mwenyezi Mungu na wakajikinga na kila linalo mghadhibisha Yeye ikiwa neno, au kitendo, au itikadi, wataambiwa: Mola wenu Mlezi kamteremshia nini Mtume wake? Wao watasema: Amemteremshia Qur'ani...ndani yake mna kheri ya duniani na Akhera kwa watu wote, na kwa hivyo wakawa miongoni mwa watu wema. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu huwalipa wema kwa maisha mazuri katika uhai huu wa duniani. Na pahala pao Akhera ni bora na pazuri zaidi kuliko waliyo yapata duniani. Na nyumba watayo ikaa wachamngu Akhera ni hadi ya raha yake!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanapoambiwa Waumini wenye kumuogopa Allah Mtukufu, «Ni kitu gani Alichokiteremsha Allah Mtukufu kwa Nabii Muhammad, (rehema na amani zimshukie?)» wanasema, «Allah Mtukufu Amemteremshia wema na uongofu.» Wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake hapa duniani na wakawalingania waja wa Allah Mtukufu kwenye Imani na matendo mema, watapata heshima kubwa ya kupewa ushindi duniani na riziki kunjufu. Na nyumba ya Akhera ni bora kwao na ni kubwa kuliko vile walivyopewa duniani. Na nyumba yenye neema zaidi ya wale wachamungu wenye kumuogopa Allah Mtukufu ni Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net