An-Nahl 16:29
النحلفَٱدْخُلُوٓا۟ أَبْوَٰبَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى ٱلْمُتَكَبِّرِينَ
Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni mabaya mno makazi ya wafanyao kiburi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi! [29]
[29] Na baada ya hayo wataambiwa: Mwisho wenu ni kuingia Motoni, na adhabu ya huko ni ya milele, haikatiki! Na mbaya mno nyumba ya Jahannamu kuwa ni makaazi ya kila mwenye kutakabari akakataa kufuata Haki na Imani ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ingieni milango ya Jahanamu. Hamtatoka humo milele. Na mahali hapo ni paovu pa kukaa wenye kiburi waliokataa kumuamini Allah Mtukufu, kumuabudu Yeye Peke Yake na kumtii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net