An-Nahl 16:28
النحلٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا۟ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوٓءٍۭ ۚ بَلَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Wale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu nafsi zao! Basi wanasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya ubaya wowote. (Wataambiwa). Hasha! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao! Basi watasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya uovu wowote. (Wataambiwa): Kwani! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyo kuwa mkiyatenda. [28]
[28] Hizaya itawashukia makafiri walio endelea na ukafiri wao mpaka Malaika walipo watoa roho, nao wamejidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na kutenda maovu, na wakasalimu amri tena baada ya inadi ndefu walipo jua hakika ya makosa yao. Wakasema uwongo kwa jinsi walivyo shituka: Hatukuwa duniani tukifanya maasi yoyote! Malaika na Manabii watawaambia: Hasha! Hakika nyinyi ni waongo, bali mmetenda maasi maovu kabisa! Na Mwenyezi Mungu, Subhanahu, anajua vyema kila dogo na kubwa mlilo kuwa mkilitenda katika dunia yenu. Hakukuleteeni faida yoyote huko kukataa kwenu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ambao Malaika watazichukua roho zao, na wao wako katika hali ya kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha. Hapo watajisalimisha kwenye amri ya Allah Mtukufu pindi wanapoyaona mauti, na watavikanusha vile walivyokuwa wakiviabudu badala ya Allah Mtukufu na watasema, «Hatukuwa tukifanya maasia yoyote.» Na wataambiwa, «Mnasema urongo! Kwa hakika, mlikuwa mkiyafanya. Allah Mtukufu Anayajua matendo yenu yote na Atawalipa kwayo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net